Kodak blac ameingia kwenye wakati mgumu baada ya kutoa kauli ambayo iliwakera mashabiki wake kuhusu mke wa marehemu Nipsey Hussle Lauren London akiwa live kwenye instagram yake.

Mashabiki wa Nipsey wameonyesha hasira zao kwa kuanza kutoa michoro ya rapa Kodak black kwenye makumbusho ya wasanii wa muziki wa trap nchini Marekani.

Kodak alisema kwa sasa Lauren ni mjane hivyo kwa kuwa anampenda sana basi yeye atakuwa mwanaume anayemfaa na atamliwaza kwa mwaka mzima kwa sababu anaamini atakuwa akimlilia mume wake Nisey  kwa kipindi chote cha mwaka mzima aliyasema hayo kupitia insta Live.

Baada ya muda mchache Kodak alirudi tena insta live na kuomba radhi, lakini kauli hiyo iliwakera wakali kama The Game na T.I ambao walioneshwa kutopendezwa  na kauli yake.

Hata hivyo kituo cha Radio Power 106 cha Los Angeles kilitangaza kutopiga muziki wake tena kutokana na kauli aliyoitoa kwenye kipindi hiki cha kuomboleza msba wa Nipsey Hussle .

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 10, 2019
LIVE: Waziri Mkuu akihutubia Bungeni Dodoma muda huu

Comments

comments