Wakili wa kujitegemea na mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Albert Msando amesema kuwa yeye si mtumwa wa siasa na wala hajamsaliti rafiki yake kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24media jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa kuhama chama ni haki yake kikatiba hivyo hajafanya usaliti wowote.

“Mimi sio mtumwa wa siasa kwani ni haki yangu ya kikatiba, na maisha yangu ya kisiasa siwezi kuyapangilia kwamba natoka chama hiki naelekea huku,”amesema Msando

Hata hivyo, ameongeza kuwa sio jambo jipya kuhama na hana mpango wowote wa kuhama CCM kwakuwa anataka kutoa mchango wake ili kuiendeleza nchi.

Donald Trump ajiondoa mpango wa Umoja wa Mataifa (UN)
Atupele Green aachwa Singida Utd