Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemtaka mkurugenzi wa wilaya ya Serengeti kufanyakazi kwa bidii kuepukana na masuala ya kisiasa.

Ameyasema hayo wilayani Serengeti mkoani Mara alipokuwa katika ziara ya kikazi, ambapo amemtaka mkurugenzi huyo kufanyakazi kwa bidii.

Aidha, rais Dkt. Magufuli amemhakikishia mkurugenzi huyo kuwa hawezi kumfukuza kazi kutokana na tuhuma zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Serengeti, Marwa Ryoba.

“Nikwambie mkurugenzi kwamba nakuhakikishia, sikufukuzi kazi, piga kazi, haya masuala ya siasa siasa yanayofanyika yasikuyumbishe,”amesema Rais Dkt. Magufuli

 

 

 

Samba Style kuchezwa Saudi Arabia
Wachezaji Ufaransa walaumiwa