Makundi makubwa ya mashabiki wa Ureno yameendelea kusheherekea baada ya timu yao ya taifa kuifunga Ufaransa katika michuano ya Euro 2016 mjini Paris.

Ureno illicheza karibia mda wote bila nyota wake Cristiano Ronaldo aliyeumia na kutolewa nje dakika 25 ya mchezo huo na baadaye kurejea na kulinyanyua kombe hilo.

Ureno imeshinda 1-0 katika muda wa nyongeza na kuwaacha mashabiki wa Ufaransa katika hali ya simanzi ndani ya dimba la Stade de France huku mitaa ya Lisbon ikirindima kwa shangwe kubwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda taji kubwa kama hilo.

Bajaji, Pikipiki, trekta kuanza kutengenezwa nchini
Serikali Yakaribisha Wawekezaji Kutoka India