Mitandao ya kijamii imefanikisha kukamatwa kwa raia wa Marekani aliyemshambulia kwa kipigo mhudumu wa Hotel ya kitalii iliyoko jijini Kampala huku akimtolea matusi kwa kisingizio cha dini.
Katika video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii, Mmarekani huyo alikuwa akimpiga makofi na ngumi mhudumu huyo ambaye hakujibu mapigo, huku mtu huyo akidai kuwa amekasirishwa na kile alichodai mhudumu amemvunjia Yesu heshima.
Jeshi la Polisi nchini Uganda liliweka video ya kukamatwa kwa raia huyo wa Marekani, na kumtambulisha kwa jina la Jimmy Tailor. Jeshi hilo liliwashukuru watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa.
“Tunawashukuru watu waliotutumia video hii ikionesha tukio lililotekea kwenye hotel ya Grand Imperial ya Kampala. Tumemkamata mtuhumiwa, Jimmy Taylor, raia wa Marekani. Anashikiliwa katika kituo kikuu cha Kampala kwa kosa la kushambulia mtu,” #CommunityPolicing imeeleza Tweet ya Polisi.
Baadhi ya Tweet za watumiaji wa mitandao ya kijamii zilimtaja Jimmy kama Mchungaji wa kanisa, huku wakihoji kama ataendelea kuwa na waumini baada ya tukio hilo.
Racist American pastor attacks Uganda hotel reception staff – in the name of Jesus! @dailykos @markos @shaunking @SkepticNikki @patrickoyulu pic.twitter.com/NHqhWYEDJ1
— Dave Bik (@davebik) August 18, 2018