Serikali imewasilisha kanuni mpya za maudhui ya vyombo vya Habari, Utangazaji na Mitandao ya kijamii kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo huku kukiwa na hofu ya uhuru wa habari kudhibitiwa.

Wadau wa habari nchini wamekuwa wakihoji ujio wa kanuni mpya kuwa zinaletwa kwa ajili ya kuminya uhuru wa habari na kujieleza au kuboresha tasnia ya utangazaji na mitandao ya kijamii nchini humo..

Aidha, Kanuni hizo mpya zinalengo la kuifanyia maboresho kanuni za Utangazaji za mwaka 2011, huku Kikao cha kwanza cha Kupokea Maoni na Mapendekezo ya wadau kuhusiana na rasimu ya kanuni za maudhui ya Utangazaji na Mitandao ya Kijamii, kikishuhudia serikali ikisisitiza kuwa Maboresho ya kanuni hizo ni kulinda Maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa madai hayo ya kudhibiti uhuru wa kujieleza hayana ukweli wowote kwani serikali inamalengo makubwa.

Hata hivyo, Wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo imetoa hadi Oktoba 6 mwaka huu kwa wadau wa vyombo vya habari, Utangazaji na mitandao ya kijamii kuwasilisha kwa maandishi maoni na mapendekezo ya kanuni hizo mpya.

Ripoti ya PPRA kutinga bungeni, taasisi 17 kuburuzwa Takukuru
HRW yaitaka dunia kulaani ukandamizaji Rwanda