Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa CCM mkoa wa Simiyu, Simon Songe amesema kuwa kambi za wanafunzi zinazowekwa mkoani humo zina manufaa makubwa.

Ameyasema hayo mkoani Simiyu wakati wa uzinduzi wa kambi ya kitaaluma ya kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Kabita mkoani humo.

Amesema kuwa kambi hizo ambazo zimekuwa zikiwekwa zina manufaa makubwa hivyo zimeweza kufanya mabadiliko makubwa katika ufaulu wa wanafunzi.

“Kwakweli kambi hizi zimeweza kuibadilisha Simiyu katika ufaulu wa wanafunzi wetu, tulikuwa nyuma sana lakini kwasasa tumepiga hatua kubwa sana,”amesema Songe

 

Video inayoonesha mateso ya jela yawaokoa
Waziri ajiuzulu na kuhama chama tawala