Jeshi la Polisi linamshikilia mlinzi wa Meja Jenerali Mstaafu, Vicent Mirataba na mfanyakazi mmoja wa benki kwa tuhuma za kuhusika kwa namna moja ama nyingine katika kupanga njama za shambulizi la Meja huyo lililotokea nyumbani kwake Ununio jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamanda Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa kwa mujibu wa muhusika amewaeleza kuwa majira ya mchana huwa analinda peke yake lindo hilo huku akiwa na silaha aina ya shortgun ambapo siku hiyo silaha hiyo aliicha wakati akifungua geti.

“Katika mazingira ya kushangaza mlinzi huyo aliweka silaha kinyume kabisa na maadili ya utunzanji wa silaha maana aliiweka juu ya kitanda, halafu akatoka mikono mitupu kwenda kuwapa ushirikiano waliyofanya uhalifu huo kwa kuwafungulia mlango na kutenda uhalifu,”amesema Kamanda Mambosasa

Video: “Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote kutoka popote atakayejaribu kuvuruga amani yetu" - Majaliwa
Video: Jambazi aliyeongoza mauaji ya Polisi 8 Kibiti auawa