Kicheche ni mnyama mdogo mwenye vituko vingi ambavyo huwashangaza watu wengi na moja ya kituko chake ni uwezo wake mkubwa wa kujamiana mara nyingi zaidi kwa siku na wana milio maalum kila wakitaka kujamiana.
Wataalamu wa wanyama wanasema kuwa kicheche anauwezo wa kujamiana mara 26 kwa siku sawa na mtu kukimbia umbali wa 360km kwa siku.
Na anauwezo wa kuishi kwa miaka 13 tu.
Kicheche ni mnyama anayepatikana katika sehemu ya jangwa la sahara Barani Afrika ukanda wa savana ni adimu sana kupatikana katika misitu mikubwa kama ya Congo na maeneo ya pwani.
Kicheche anafanana sana na Nguchiro ana urefu wa sentimeta 60, urefu huo ukijumlisha mwili na mkia wake ambapo mkia pekee una urefu wa sentimeta 20.
Chakula kikubwa cha kicheche ni ndege, nyoka, mijusi, chura, wadudu na wanyama wengine wadogo kama panya nk.
Unaambiwa wakati wa kukabiliana na maadui mnyama huyo hutoa harufu kali kwa kujamba na kuwafanya maadui kugaili kumkamata na wazungu humuita “Father of stinks kutokana na harufu kali anayo toa wakati akijihami na maadui.
Pia kicheche ana tabia ya kuinua mkia wake kwa kubinua mgongo ili aonekane mkubwa baada ya kumuona adui yake kwa lengo la kumtisha na mara nyingi hupenda kula kila wakati.