Msanii anayeonesha dalili za kuifuata A-List ya wasanii wakali Tanzania na Afrika Mashariki, Dee Pesa ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Kanjubahi’, akiwa na Jack Chant na Ebe Nation.

Kupitia wimbo huu, Dee Pesa ametambulisha aina mpya ya muziki wake alioubatiza jina ‘Vigoma Rap’.

“Nimechanganya trap na ngoma za asili kwenye mdundo mmoja ili kupata ladha mpya inayowawavuta pamoja watu wanaopenda muziki wa asili ya Afrika na wale wa ughaibuni,” Dee Pesa ameiambia Dar24.

Msanii huyo hivi sasa yuko chini ya label ya StarTraits.
Enjoy!

Kikwete avunja ukimya, ataka aachwe apumzike, "nimechoka"
Ligi Daraja La Kwanza Tanzania Bara Kuunguruma Tena