Profesa Jay ameachia rasmi video ya wimbo wake mpya ‘Kibabe’, iliyofanyika nchini na kuongozwa na muongozaji anayefanya vizuri katika tasnia hiyo hivi sasa, Hanscana.
Video inaonesha mazingira ya kuvutia ikiwa ni pamoja na eneo la mbuga za wanyama za Mikumi, jimbo ambalo gwiji huyo amepewa dhamana na wananchi kuwa mbunge.