Mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini, Charles Mwijage amesema mtu anayefanyakazi ndiye anayeleta kazi kauli ambayo amemtolea mfano Rais John Pombe Magufuli kuwa ndiye aliyeleta elimu bure na kusababisha wanafunzi wengi wengi kujaa madarasani.

Mwijage akichangia hotuba ya Waziri wa Nchi tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Selemani Jafo katika mapitio ya makadirio ya mapato na matumizi ya wiza hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/20 na wizara ya Utawala Bora amesema hali ya shule kwa sasa zipo vizuri kutokana na kuwapo na miundombinu bora.

Video: Dkt. Ndugulile awatahadharisha wananchi kuhusu Dengue
Al-Shabaab wateka madaktari bingwa wa Cuba

Comments

comments