Abuu Athman Amri, mtoto wa marehemu Athumani Amri maarufu kama Mzee Majuto amekanusha taarifa zinazodai kuwa mama yake amefukuzwa nyumbani alikokuwa akiishi na marehemu mume wake kama ambavyo amekuwa akizungumza kwenye vyombo vya habari .

Abuu amesema mama yake amekwenda Dar es salaam kutembea na kupumzika katika kipindi hiki kigumu ambacho amempoteza mume wake.

Amezungumza hayo akiwa nyumbani kwao Tanga eneo la Donge alikokuwa akiishi marehemu Majuto na mke wake pindi akifanyiwa mahojiano na chombo cha habari cha Dar 24.

” Mama hayupo nyumbani ameenda matembezi kidogo, ameenda kupumzika kwa sababu ya majozi ya mumewe, kukaa mwenyewe anajiona mpweke, maanake alituaga anaenda Dar mara moja kupumzika, mama hapa ni kwake” amesema Abuu.

Ngome ya Mbowe yazidi kutikiswa, mwingine atimkia CCM
Tuzo za MTV – VMAs: Orodha kamili ya washindi