Marion Suge J. Knight, mtoto wa aliyekuwa Bosi wa lebo ya Death Row Records, Suge Knight ameendelea kudai kuwa Tupac bado yuko hai na kwamba anaishi kwa siri nchini Malaysia.

Inafahamika kuwa Tupac aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 1996, Las Vegas nchini Marekani, lakini Marion anadai kuwa aliondolewa kwa nguvu za giza za ‘Freemasons (Illuminati), na kwamba bado yuko hai. Baba wa mtoto huyo, Suge Knight, ndiye aliyekuwa anasimamia kazi za Tupac na mmoja wa mashuhuda wa tukio la kuuawa kwake.

Marion ameendelea kusisitiza kuwa Tupac alinusurika katika tukio hilo la kupigwa risasi.

Hivi karibuni Suge alizua kizazaa baada ya kuweka kwenye Instagram kipande hicho cha video kinachomuonesha mtu ambaye amedai kuwa ni Tupac, akidai anataka kuidhihirishia dunia ukweli wa jambo hilo, kabla ‘hawajamuondoa’.

“Updated video from Malaysia source #killuminati,” aliandika kwenye video hiyo, akimaanisha kuwa ni video ya hivi karibuni kutoka Malaysia.

 

View this post on Instagram

 

Updated video from Malaysia source #killuminati

A post shared by Suge J Knight (@sugejknight) on


Aidha, baada ya kuweka kipande hicho cha video, baadhi ya watumiaji wa mtandao huo walihamia Twitter wakidai kuwa Instagram imefungwa kwa muda usiku huo baada ya mtoto wa Suge kuweka ‘video ya Tupac’.

Marion alianza kuzua hali ya taharuki Oktoba 2 mwaka huu alipoweka picha inayomuonesha ‘Tupac’ akiwa katika hali ya umri mkubwa zaidi, akiwa na 50 Cent na nyingine akiwa na Beyonce, na kuandika kwa kutumia msemo mpya wa 50 Cent, “get the strap y’all see it.” na nyingine “He never left us. They’ll be after me soon smh. For y’all tho100%”.

Akimaanisha kuwa wote mmeona. Hajawahi kutuacha. Watanitafuta [kunimaliza] hivi punde.

 

View this post on Instagram

 

@50cent get the strap y’all see it

A post shared by Suge J Knight (@sugejknight) on

Aliendelea kusisitiza kuwa yuko katika hali nzuri kiakili na kiafya, na kwamba hajatumia kilevi chochote kuyasema hayo.

Hata hivyo, Septemba 2017, chanzo kimoja ambacho kilihusika katika mahojiano na Jeshi la Polisi la Los Angeles, kililiambia jarida la People kuwa 2Pac aliuawa na maadui wa kibiashara wa Suge Knight.

Watumiaji wengi pia wameonesha kutokubaliana na picha hizo wakidai huenda zimetumia teknolojia kuziunganisha. Lakini Marion anaendelea kufanya mahojiano na vyombo vikubwa vya habari kuhusu hili alilolianzisha kwenye mitandao.

Hadi sasa, vyombo vya dola nchini humo bado havijatoa tamko la kumuonesha muuaji wa Tupac.

Mbappe, Alexander-Arnold, Rodrygo Silva kuwania Kopa Trophy
Ndege walevi wazua gumzo Marekani