Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia amekabidhiwa rasmi kadi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ofisi za chama hicho Kinondoni zilizopo jijini Dar es salaam.

Mtulia alitangaza kujivua ubunge na nafasi zote ndani ya chama hicho, disemba 2 mwaka huu, ambapo alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa lengo la kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dkt. Magufuli za kuliletea maendeleo taifa.

Video: Mtulia amwaga mboga CUF, afunguka sababu za kuacha ubunge na kuhamia CCM

Usiku wa Kitendawili kufufua upya Uzalendo na Utaifa
Aliyesambaza picha za majengo UDSM atiwa mbaroni