Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amezungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la Maliasili na Utalii katika maonesho ya 43 kwenye viwanja vya Sabasaba ambapo ametaja fursa mbalimbali kwa wawekezaji zinazopatikana kwenye sekta hiyo ya misitu na utalii.

Pia ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha watanzania kufanya utalii wa ndani ili wawe mabalozi wazuri wa vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania, akiongezea hayo amegusia hifadhi ya msitu wa Magamba ambao unapatikana mkoa wa Tanga wilayani Lushoto na kutoa rai kwa watanzania kujitokeza kwa wingi katika ziara ya ndani ya utalii iliyoandaliwa na Mawakala wa huduma za Misitu, TFS katika kipindi hiki cha sabasaba ambapo watafanya ziara hiyo itakayoanzia katika viwanja vya sabasaba tarehe 12, julai mwaka huu.

Kuna watu wanaropoka tu huko- Uhuru Kenyatta
Video: TFS yaandaa ziara ya utalii hifadhi ya Magamba Lushoto