Aliyekuwa Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye, ameikosoa vikali miradi ya Rais Dkt. Magufuli akisema kuwa inatumia gharama kubwa.

Ameyasema hayo hii leo bungeni Mjini Dodoma, ambapo amesema kuwa miradi hiyo itachukua muda mrefu hivyo itabidi italazimu kutumia fedha za serikali, kitu ambacho kitasababisha kudorora kwa huduma za kijamii.

Nape ametolea mfano miradi mitatu ukiwemo mradi wa reli ya kati ambao utagharimu kiasi cha dola bilioni 15, mradi wa uzalishaji wa umeme ambao unatarajiwa kugharimu dola bilioni 5 na ule wa shirika la ndege Tanzania ambapo miradi yote hiyo itagharimu dola bilioni 21.

“Hapa miradi hii haina maana kuendelea nayo kwani itatuingiza kwenye matatizo ya kutokopesheka kwakua tutakuwa tumevuka kiwango cha kukopesheka,”amesema Nape

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 11, 2017
Malinzi, Mwesigwa wakwama mahakamani