Kumekuwa na tetesi juu ya mahusiano kati ya mkongwe wa muziki wa hiphop Nasir Bin Olu Dara Jones maarufu kama Nas na rapa kutoka katika lebo ya ‘Young Money’ Nick Minaj lakini wawili hao bado hawajaweka wazi kuhusu mahusiano yao.

Uvumi wa wawili hao kuwa katika mahusiano umechukua sura mpya baada ya Nick Minaji kuweka video katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa karibu sana na Nas wakati wa Sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Nas.

Nick Minaji hajawahi kuficha upando wake kwa Nas kwani akihojiwa katika kipindi cha Ellen DeGeneres Nick Minaji alisema baada ya kuachana na Meek Mill asingependa kuwa na mwanaume yeyote mpaka upite mwaka lakini anaweza kutoa nafasi kwa Nas pekee.

Itazame video hiyo inayo mounyesha Nick Minaj akiwa na Nas hapa chini;

 

 

Wazee wa Kigoma wamjia juu Spika Ndugai
Kamati ya bunge yakwama kutoa ripoti ya Lissu