Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kupungua kwa gharama za vyakula hasa vinavyotokana na mazao kumetajwa kuwa ni kichocheo cha kupungua kwa mfumuko wa bei uliofikia asilimia 3.8 Aprili ikilinganishwa na asilimia 3.9 ya mwezi Machi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa mfumuko wa bidhaa za vinywaji baridi umepungua hadi asilimia 3.6.

“Kupungua kwa kasi ya mfumuko wa bei haina maana kwamba leo au kesho utaenda dukani ukute bidhaa zimeshuka bei,”amesema Kwesigabo

Hata hivyo Takwimu hizo zimetolewa wakati kukiwa na mjadala mkubwa wa kuhusu kupanda kwa bei za mafuta ya kula na sukari.

 

Lusinde adai serikali imeshindwa kudhibiti matumizi ya fedha
Wachimbaji 6 wa madini wafukiwa na kifusi