Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ameendelea na ziara yake ya kutembelea kila kijiji katika kila kata zilizopo jimboni mwake, ambapo leo ametembela kijiji cha ujungu Kata ya Mekente na kukuta hali ya shule ya msingi Ujungu katika kijiji hicho si nzuri.
Waziri Mwigulu ameshuhudia ubovu wa madarasa matatu ya shule hiyo yakiwa mabovu kabisa na yenye nyufa kubwa ambayo ni hatari sana kwa usalama wa wanafunzi huku madarasa hayo yakiwa hayana sakafu kabisa.
Pia shule hiyo ikiwa na walimu 9 na nyumba za walimu nne ambazo walimu hukaa pamoja katika nyumba hizo huku vyumba vya madarasa vilivyobaki navyo si vyakulizisha sana.
Waziri Mwigulu amewahidi walimu wazazi na wanafunzi wa shule hiyo kuwa amelichukua jambo hilo na kwa kuanzia anatoa mifuko 200 ya saruji na anapofika mjini ataongea na marafiki zake waweze kutengeneza mkakati wa kushurikia kujenga madarasa hayo na nyumba za walimu, huku hakiwasifia kwa shule hiyo kutoa wanafunzi kwenda shule za vipaji maalumu kama Mzumbe ya morogoro.