Serikali imepokea msaada wa vitabu vya Sayansi milioni moja na thelathini kutoka kwa balozi wa wa India nchini.

Akizungumza mapema hii leo jijini Dar es salaam wakati wa kupokea msaada huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Joyce Ndalichako amesema kuwa msaada huo utasaidia kuweza kuinua masomo ya sayansi nchini.

Amesema kuwa bila kujali wanafunzi wanatoka wapi au mahala wanaposoma kwa sasa hivi watapata elimu bora.

“Sayansi ndio imekuwa kipaumbele sana kwa Serikali ya awamu ya tano, ili tuweze kufikia uchumi wa viwanda ni lazima masomo ya Sayansi yatiliwe mkazo,”amesema Ndalichako

Hata hivyo, ameongeza kuwa msaada huo uliotolewa na ubalozi wa India hapa nchini unadumisha uhusiano uliopo.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 11, 2017
Picha: Rais Magufuli akutana na Bill Gates Ikulu Dar es salaam