Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema watanzania wengi ambao ni wasomi wanashida ya kuwadharau wale ambao hawajosa kama wao, pia amelaumu waandishi wa habari kwa kufanya jambo la CAG kuwa kubwa.

”Shida yenu nyinyi mtu akishasoma anawaona nyie wengine mbuzi tu, anawaona kama nyie akili zenu mbovu hamtoshi, sasa waandishi baada ya kuliweka vizuri mnakuza jambo hili, katiba ipi iliyomruhusu mtu awe anadharu wenzake”. amehoji Ndugai.

CAG hakutakiwa kulitukana bunge kwa lugha ya rejareja katika kutekeleza majukumu yake kwani bunge hufanya majukumu yake kufuatana na kanuni za bunge.

Amesisitiza kuwarudisha wasomi wanapotakiwa kuwa ili waone wengine ni wenzao nao ni binadamau wanapofanya mambo wamefikiri na sio dhaifu.

Amesema hivyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amezungumza msimamo wao kama wabunge mara baada ya CAG kutoa kauli ya kuwa bunge ni dhaifu na kusisitiza kuwa ataendelea kutumia kauli hiyo.

Viongozi wa Serikali ya Al-Bashir wakamatwa, wananchi wapewa makucha
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 15, 2019