Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Darasa la saba kwa wanafunzi waliofanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2018 ambapo matokeo hayo yameongezeka kwa asilimia 4.96 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa, Dkt. Charles Msonde amesema kuwa ufaulu umetajwa kuongezeka kwenye masomo ya Hisabati, Sayansi, Maarifa ya jamii ambapo katika masomo hayo somo la Kingereza limeelezwa kuwa na ufaulu wa chini ya asilimia 50 ukilinganisha na masomo yote.
“Tathmini ya awali kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.9% ikilinganishwa na 2017, pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza uko chini sana tofauti na masomo mengine, chini ya asilimia 50.”amesema Dkt. Msonde
Aidha, Jumla ya watahiniwa 733,103 kati ya 943,318 wamefaulu mtihani huo wa kuhitimu elimu ya msingi uliofanyika septemba 5 na 6 mwaka huu sawa na asilimia 77.72 kati yao wasichana 382, 273 na wavulana 350,273.
-
Makamba aeleza alivyohojiwa sakata la Mo Dewji, ‘sikukamatwa
-
Lowassa ajibu taarifa za kuwalinda wabunge 8 wasitimuliwe
-
Video: MSHTUKO ajali nyingine mbaya ikiua watumishi, SAKATA LA MO: Polisi wamhoji January kwa dakika 30