Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa ni kweli Tanzania ni masikini lakini zinafanyika jitihada kubwa za kuweza kutatua tatizo la maji nchini.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa tayari rais Dkt. Magufuli alishaongelea suala hilo wakati wa akihutubia bunge.

Amesema kuwa changamoto kubwa ambayo ilikuwa ikisumbua ni uhaba wa rasilimali fedha hivyo kwasasa wanaelekea kutatua tatizo hilo kwani wanashirikiana wa mashirika mbalimbali ya kimataifa.

“Ni kweli kwamba nchi yetu ni masikini lakini rais Dkt. Magufuli alishaongelea jambo hilo akiwa anahutubia bunge, na akasema anaanzisha mpango wa kumtua mama ndoo kichwani,”amesema Prof. Kitila

Watu 65 wafariki dunia kwa joto kali
Fahamu alama za kucha na maana zake kiafya