Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima kumkamata mtu mmoja ambaye anajulikana kwa jina la King’anya ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

Ametoa agizo hilo mapema hii leo mkoani humo wakati wa ziara yake ya kikazi mara baada ya kupata malalamiko kutoka wananchi.

“Huyu King’anya kama yupo hapa ajitokeze, yuko wapi, nakuagiza mkuu wa mkoa umtafute na kumkamata ili aweze kujibu na kutoa maelezo ya tuhuma hizi,”amesema Rais Dkt. Magufuli

 

Marcelo aikana Juventus FC
Geoffrey Kondogbia, Frederic Nimani ruhsa kucheza Afrika ya kati