Mkuu wa Wilaya ya Arumeru iliyopo mkoani Arusha, Jerry Muro ametoa onyo kali kwa kijana yeyote atakayemtia mimba mtoto wa kike kuwa atasota jela miaka 30.

Ameyasema wilayani Arumeru jijini Arusha alipokuwa akizungumza na viongozi wa wilaya hiyo, ambapo amesema kijana yeyote atakayediriki kufanya hivyo maisha yake yote yatakuwa ni jela.

“Ninasema hivi mimi kama mkuu wa wilaya ya Arumeru, natangaza kuwa kijana yeyote atakayempa mimba mtoto wa kike chamoto atakiona,”amesema DC Muro

Huyu ndiye mkuu wa mkoa bora kwangu- JPM
Video: Mkurugenzi Lutengano ataja mambo manne wilayani Magu