Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa atashangaa sana endapo wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanastahili kupata mikopo watafungua vyuo na kukosa mikopo hiyo.

Ameyasema hayo hii leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao, pia na baadhi ya wakuu wa mikoa, ambapo amesema kuwa toka tarehe 29 ya mwezi uliopita alikuwa ameidhinisha fedha hizo za mikopo zaidi ya bilioni 145 hivyo anategemea wanafunzi wakifungua vyuo vikuu watapata fedha hizo.

“Toka mwezi uliopita kwenye tarehe 29 nilipitisha bilioni 147 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaostahili kupata mikopo, nitashangaa sana kama kutakuwepo na wanafunzi wapo kwenye orodha ya kupata mikopo na mikopo watakuwa hawajapata mpaka wanafungua vyuo, mimi najua nimeshaidhinisha hizo fedha sitapenda kuona wanafunzi wanafungua vyuo na kuanza kuteseka wakati fedha zipo,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, Vyuo Vikuu nchini Tanzania vinatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu kutokana na ratiba iliyotangazwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU)

Sanga atangaza kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi
Shahidi: Tuliahidiwa milioni 17 kila mmoja kumuua Msuya