Kamishna wa Kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amelikataa ombi la Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) la kutaka kufanya maandamano ya kwenda kufanya maombi huku akisema maombi yote yanafanyika makanisani na misikitini.

Tofauti na hilo pia Kamanda Mambosasa amepiga marufuku maandamano ya Chama cha Wananchi CUF ambayo yalikuwa yanatarajiwa kufanyika siku ya jumapili kwaajili ya kuwapokea wabunge wanaotoka bungeni mkoani Dodoma.

“Wananchi wanaoisha Kanda Maalum ya Dar es salaam niwaombe watii sheria  bila shuruti, hakuna maandamano yeyote yatakayoruhusiwa hata wale wanaotaka kufanya maombi wakafanye makanisani na misikitini,”amesema Kamanda Mambosasa

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 16, 2017
Video: Jeshi la polisi kula sahani moja na wahalifu wa mitandaoni