Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kumkata mtu aliyekuwa akijifanya Askari Polisi na kuwakamata wananchi mbalimbali huku akiwatoza fedha kwa madai kuwa ni faini ya makosa waliyoyafanya.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa, ambapo amesema kuwa kukamatwa kwa mtu huyo ambaye alikuwa akijifanya ni polisi kumetokana na ushirikiano kati ya jeshi hilo na wananchi.

“Kukamatwa kwa mtu huyu, ambaye alikuwa akjifanya Askari Polisi kunatokana na ushirikiano uliopo kati ya polisi Dar es salaam na wananchi, hivyo nawaomba wananchi tuendeleze ushirikiano huu,”amesema Mambosasa

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 7, 2017
IGP Sirro atoa wito kwa wanasiasa