Leo Septemba 15, 2016 Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Twaweza imetoa matokeo ya utafiti uitwao ‘Rais wa Watu? Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano’ ambapo wamesema kuwa Wananchi wanakubali hatua zinazochukuliwa na serikali mpya inayoongozwa na Rais Dk. Magufuli, hususani kuhusu uondoaji wa wafanyakazi hewa, sera ya elimu bure na usimamishwaji wa watumishi wa serikali kutokana na makosa mbalimbali.

Kufuatia ripoti hiyo, Profesa Mwesiga Baregu ameeleza kukosa uhakika na matokeo hayo ya utafiti kwani ulifanyika mwezi wa 6 huku mambo mengi yakitokea ndani ya miezi mitatu iliyopita ambayo yamebadilisha mtizamo wa Watanzania kuhusu Rais.

Prof. Baregu pia amesema kuwa utafiti huo umeonyesha asilimia 70 ya Watanzania hawakuwa na uelewa wa kisiasa. Tazama video

Zanzibar Waandika Historia Afrika Mashariki Na Kati
Roy Keane: Guardiola Anapaswa Kuitwa “The Special One”, Sio Mourinho