Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa yuko tayari kuachia madaraka ya chama hicho endapo atapatikana mtu mwenye sifa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa CUF inafuata demokrasia hivyo ikiwa kuna mwanachama hai mwenye sifa ajitokeze kuwania uenyekiti kwani muda ukifika wa uchaguzi hakuna sababu ya kung’ang’ania madaraka.

“Nitampisha atakayekuja kuwania nafasi ya uenyekiti ili mradi tu awe na sifa za uenyekiti na akubalike kwenye chama, sitokuwa na pingamizi lolote,”amesema Prof. Lipumba

Amesema kuwa mpaka sasa hakuna mtu aliyejitokeza kuwania uenyekiti wa chama hicho ambaye atapitishwa pia kuwa mgombea urais 2020.

Akizungumzia suala la Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kutajwa kuitwa CHADEMA, amesema kuwa hatua hiyo haitakiathiri chama hicho kwa sababu CUF bado inakubalika Zanzibar na kusisitiza kuwa chimbuko la CUF ni Zanzibar, hivyo CHADEMA hawawezi kuiua CUF Zanzibar.

Hata hivyo, Prof. Lipumba alitangaza kujiuzulu uenyekiti, Agosti 5, 2015 lakini baada ya mwaka mmoja akatengua uamuzi huo na kutangaza kurejea katika wadhifa huo jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad

Video: Chama cha CHAUMMA chatoa rambirambi kufuatia ajali ya MV Nyerere
Didier Ndong ajifukuzisha Sunderland