Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo amefanya mabadiliko madogo ya Makatibu Wakuu ambapo amemteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Aidha, Prof. Mkumbo anachukua nafasi ya Mbogo Futakamba aliyestaafu, kabla ya uteuzi huo Prof. Kitila alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM).

Pia Rais Dkt. Rais Magufuli amemteua Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, kabla ya hapo Dkt. Akwilipo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi kuhamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Hata hivyo wateule wote wanatarajia kuapishwa kesho tarehe 5/4/ 2017 Ikulu Jijini Dar es salaam na kuanza kazi mara moja.

JKT Ruvu Waelekea Bukoba
Wimbo wa Azma aliowakutanisha Sugu na Izzo Bizness wavuja, afunguka