Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezindua Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo chini ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Uzinduzi huo umefanyika Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali inahusika na mambo manne ambayo ni Utawala Bora, Maendeleo ya Vijana, Afya ya Mama na Mtoto na Maendeleo ya Wakulima Wadogo Wadogo
Aidha, Rais Magufuli amesemsifu na kumshukuru rais mstaafu, Jakaya Kikwete kwa kuanzisha Taasisi hiyo na kuahidi kwamba Serikali ya awamu ya 5 itafanya kazi bega kwa bega na Taasisi hiyo
Kwa upande wake Rais Mstaafu Kikwete amesema kuwa kwa sasa Taasisi hiyo itaanza kujishughulisha na masuala ya Afya kwanza.
Hata hivyo, Rais Magufuli ameomba watu mbalimbali ikiwemo Mabalozi wamuunge mkono Kikwete katika Taasisi hiyo kwa kuwa anamuamini.