Mirerani, Simanjiro Mkoani Manyara, Leo katika hafla ya uzinduzi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita 3 kwenda juu uliojengwa kuzunguka eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite, Rais Magufuli amempatia milioni 100 za Kitanzania aliyegundua madini ya Tanzanite, anayefahamika kwa jina la Jumanne Ngoma.
Jumanne Ngoma, ni mtu wa kwanza kugundua madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee, hivyo Rais Magufuli amemshukuru na kuahidi kumpa fedha hizo Mzee Ngoma ambaye kwa sasa anasumbuliwa na tatizo la miguu ambayo imepooza.
Kama namna ya kumshukuru JPM amesema Mzee Ngoma atatumia fedha hizo kwa matibabu na matumizi yake mengine ya kujikimu kimaisha.
Magufuli amesema pesa hiyo itaingia katika akaunti yake siku za hivi karibuni mara baada ya mzee huyo kutoa taarifa kuhusu akaunti zake za benki.
Aidha amemshukuru mzee Ngoma kwa ujuzi wake na kuifanya Tanzania kuwa ya pekee kwa kuyagundua madini ambayo yanapatikana Tanzania pekee.