Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, IGP Simon Sirro kumsimamisha kazi kamanda wa polisi wa Wilaya ya Sumbawanga, Polycarp Urio kwa madai ya kushindwa kutekeleza maagizo aliyopewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Oktoba 6, 2019 akiwa ziarani mkoani Rukwa, ambapo alimpigia simu IGP Sirro na kumtaka kumsimamisha kazi kamanda huyo.

Septemba 30, 2019 alipewa maelekezo ya kuwahamisha kazi askari tisa wa kituo cha polisi Laela kutokana na tuhuma za uonevu na kuomba rushwa lakini hakufanya hivyo.

Tembo sita wafa maji wakijaribu kuokoana
Spurs yapigwa 3-0, Connolly atakata