Leo katika uzinduzi wa Kituo cha mabasi cha kisasa Mkoani Morogoro, Msamvu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewataka viongozi kutengeneza mkakati wa kuwawezesha wafanyabiashara wadogowadogo kuruhusiwa kufanya biashara ndani ya kituo hiko ambapo awali wafanyabiashara hao walipigwa marufuku.
Magufuli amesema hawezi kufungua stendi yenye ubaguzi kwa sababu alichaguliwa na watanzani wote wenye maisha ya chini, maisha ya juu na maisha ya kawaida.
”Mimi siku zote nimekuwa nikisimama kwa ajili ya watanzania wa hali ya chini inawezekana leo msifurahi kwanini mmenialika kuja kufungua, laikini dhamira yangu inanituma mimi kama rais, tumeanza kutoa pesa kwa ajili ya kujenga standi mbalimbali katika mikao mbalimbali lakini tumeanza kujenga stendi nzuri kwa sababu ya kujifunza kazi nzuri iliyofanywa hapa”.
-
Video: Rais Magufuli kufungua kituo cha mabasi cha kisasa Msamvu, Morogoro
-
Kidato cha sita kuanza mtihani wa Taifa kesho
”Huo ndio utanzania ninoutaka, huo ndio uwekezaji ninoutaka unaoweza kuwanufaisha wote, tumeanzisha utaratibu wamachinga wote katika maeneo mbalimbali wasibuguziwe wasifukuzwe lakini wapewe vitambulisho mtakuwa mmewajengea maisha yao” ameongezea Magufuli.
Aidha Magufuli amesema inawezekana mabasi yanayopita hapo sio abiria wote ni matajiri wenye uwezo wa kula mgahawani hivyo uwepo wa wafanyabiashara hao wadogo kutawawezesha wa hali ya chini kupata chochote.
Ameongezea kuwa fedha isiyojali wananchi maskini ni fedha haramu ili fedha iwe nzuri na ilete faida kwa watanzania wote ni lazima kutengenezwa utaratibu mzuri utakaounufaisha watanzania wote.