Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein amewafunda wanafunzi wa shule ya msingi akiwataka kuachana na mambo yasiyoendana na umri wao bali wazingatie masomo.
Akizungumza katika shule ya msingi Kihinani, wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi ambapo aliweka jiwe la msingi la jengo la shule hiyo, Dkt. Shein aliwaeleza wanafunzi hao umuhimu wa elimu na kuwasimulia jinsi ambavyo wao walizingatia ushauri waliopewa na wazazi wao kuhusu kuishika elimu.
Rais Shein ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo, aliwapongeza wanafunzi wa kike kwa namna wanavyopiga hatua katika sekta ya elimu na kuwazidi wanafunzi wa kiume, tofauti na ilivyokuwa awali.
Angalia video hii kufahamu kiundani mafunzo na nasaha alizozitoa Rais Shein kwa wanafunzi, wazazi na walimu wa kike: