Wakati machafuko yakiendelea huko Afrika ya Kusini kuwaondoa wageni, mwanamuziki wa kizazi kipya Raymond Hassan ‘Rayvanny’ ametunga wimbo wa Afrika kuonesha kusikitishwa na tukio hilo.
Msanii huyo ambae alishawahi kufanya nyimbo na baadhi ya wasanii wa nchi hiyo akiwemo Dj Buckz pamoja Maphorisa kupitia wimbo wa makulusa amekemea kitendo hicho kwamba ni ukatiri na udhalilishaji kwa Afrika wenyewe.
Rayvanny anakuwa miongoni mwa wanamuziki wa Afrika kuoneshwa kukerwa na tukio hilo, mwanamuziki maarufu nchini Nigeria Tiwa Savage ambae alikuwa anategemewa kutumbuiza katika tamasha la DSTV show case Jijini Johannessburg amehairisha kwenda kutumbuiza kutokana na vurugu zinazoendelea.
Kwa hatua nyingine moja ya wasanii wakongwe hapa nchini Fid Q amehairisha kwenda kutumbuiza hivi karibuni nchini humo kutokana na wanyeji kuona wageni wanaenda kuchukua fursa zao na wao kubaki bila ajira.
Aidha, Madee nae aliamua kufututa nyimbo zake zote katika youtube yake alizowahi kufanya nchini Afrika ya kusini na kutoa amri ya kutopigwa katika kituo chochote cha runinga kwani itakuwa inaonesha mandhari ya nchi hiyo.
Machafuko hayo ya Afrika kusini yanatokana na wageni kutaka raia wa kigeni waondoke katika nchi yao, wakidai kwamba wageni wanachukua ajira zao na wao kubaki bila ya kazi.