Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wananchi wa Dar es salaam kuunga mkono kampeni ya kujenga ofisi za Waalimu ambazo zitaweza kuimarisha na kuboresha mazingira ya ufundishaji na kuongeza uwezo wa ufaulu kwa wanafunzi.

Amesema kuwa ni wajibu wa kila mzazi kuchangia katika kampeni hiyo kwani inafanyika kwaajili ya kuinua elimu ya Tanzania kwa wote na si kwa mkoa wa Dar es salaam pekekee.

“Tunatarajia kujenga Ofisi 402 za Waalimu jijini Dar es salaam, tunafanya hivi kwaajili ya kuboresha elimu yetu kwani kuboresha mazingira ya waalimu tutakuwa tumefanikisha azma ya Serikali ya kutoa elimu bure,”amesema Makonda.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuchangia katika elimu bila kujali wanatoka mkoa gani kwani elimu haina mipaka, hivyo ameviomba vyombo mbalimbali kushiriki katika Kampeni.

 

 

Video: Takataka zageuka dili, sasa kuzalisha mbolea
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 1, 2017