Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albart Chalamila akiwa ameambatana na Afisa Elimu ya Msingi Mkoa wa Mbeya amefanya ziara ya ya kushtukiza kwenye shule ya Msingi Mwakibete na Uhuru, baada ya kupata taarifa za uonevu, unyanyasaji na matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na Walimu Wakuu hususani katika shule ya Msingi Mwakibete, ambaye amepeleka taarifa za uongo kwa Afisa Elimu Msingi na kuwahamisha walimu wawili, ambapo ni Mwalimu Elizabeth Mpondo na Mwalimu Aurelia Njee.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albart Chalamila amewataka Walimu Wakuu wa shule za msingi Jijini Mbeya kuacha kujifanya miungu watu na kuwanyanyasa Walimu, na kutoa agizo la kurejeshwa kwa walimu wawili wa shule ya msingi Mwakibete kwenye viyuo vyao vya kazi, ambao wamehamishwa baada ya Mwalimu mkuu wa shule kutoa taarifa za uongo kwa Afisa Elimu.

Prof. Palamagamba atoa neno kwa Mawakili
Mwanamke mwenye asili ya Tanzania aweka historia Pakistan