Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu, Zelote Stephen amesema kuwa wale wote waliokula fedha za mradi wa TASAF wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria kwani fedha hizo zimetolewa na Serikali kunusuru Kaya maskini ili kuwasaidia wananchi wasio na uwezo waweze kujikwamua.
“Mimi nina taarifa kwamba fedha za ufuatiliaji wa TASAF zikifika tu katika Ofisi ya Mkurugenzi, kama zimefika asubuhi basi mchana tu hakuna senti tano, zote zimeshanyanganyiwa na hatimae makusudio ya fedha zile hayatimii na ufuatiliaji haufanywi,” amesema.