Real Betis aliwashangaza mashabiki wengi waliojitokeza katika uwanja wa Santiago Bernabeu kushuhudia mchezo wa ligi ya Hispania La Liga, ambao Real madrid ilijikuta ikiambulia kipigo cha bao 1-0.

Hii ni mara ya kwanza kwa Real Betis kupata ushindi dhidi ya Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu tangu miaka 19 iliyopita.

Pamoja na kurejea kwa Christiano Ronaldo aliyekuwa amefungiwa kucheza michezo mitano, Madrid walishindwa kuamini kilichotokea baada Antonio Sanabria kupachika bao la ushindi kwa Real Betis dakika za lala salama nakuifanya Madrid kuendelea kuachwa mbali kwa pointi na Barcelona.

Tazama video fupi ya mchezo huo hapa chini;

 

Video: Usione nimekaa kihasara nakula matunda yangu-Nikki wa Pili
Lema kupandishwa kizimbani oktoba 24