Rapa na mmiliki wa lebo ya muziki ya ‘Maybach Music Group’ (MMG) William Leonard Roberts II maarufu kama Rick Ross ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Lamborghini doors’ akimshirikisha Meek Mill pamoja na Anhtony Hamiltony.

Wimbo wa Lamborghini doors unatoka katika albamu mpya ya tisa ya Rick Ross inayoitwa ‘Rather You Than Me’ iliyotoka rasmi tarehe 17 mwezi Machi mwaka huu.

Rick Ross amemshirikisha Meek Mill katika wimbo huo huku ikiwa ni siku chache tangu kuwepo kwa tetesi za rapa huyo kutofurahishwa na kitendo cha Meek Mill ambaye ni msanii wake anayetoka katika lebo ya MMG kupanda jukwaani katika usiku wa pambano la Floyd Mayweather Jr na Conor McGregor na kuimba akiwa na 50 Cent ambaye ni adui wa Rick Ross kwa muda mrefu.

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 3, 2017
Mimba za utotoni zakithiri mashuleni