Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amemkingia kifua Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Humphrey Polepole dhidi ya tuhuma zinazotolewa na vyama vya upinzani.

Ameyasema hayo Jimboni Chalinze alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa wapinzani wanaomtuhumu Polepole hawana hoja.

Amesema kuwa Katibu huyo anafanya kazi nzuri ya kuimarisha chama hivyo, watu wanaomtolea tuhuma ni lazima wakajipange upya.

“Unajua ukitaka kumuua Mbwa kwa sisi Waswahili ni lazima uanze kumtungia majina mabaya, utasema huyu mbwa anatabia mbaya, hivyo hawa wapinzani inabidi wajipange,”amesema Ridhiwani Kikwete

 

Meli yawaka moto katika Bandari ya Bagamoyo
Cardi B ajitoa kumtupa chini mwanaye apigane na shabiki wa Nicki Minaj