Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kitendo cha baadhi ya viongozi wa upinzani kuhamia CCM ni sahihi kwani kila mtu ana haki ya kuchagua pale anapoona ni sahihi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo aamesema kuwa viongozi hao wana haki ya kuhamia kwenye chama ambacho wanaona ni sahihi.

“Kwa hili linaloendelea, la baadhi ya viongozi wa upinzani kuhamia CCM, ni jambo jema kwakuwa wameona huko walikokuwa mambo hayaendi sawa, sisi huku tunawakaribisha nyumbani,”amesema Ridhiwani

Jinsi ya kufanya kazi na Bosi msumbufu
Max Meyer anasa kwenye rada ya Crystal Palace

Comments

comments