Rapa Roma Mkatoliki ameachia video ya wimbo wake ‘Zimbabwe’ ukiwa ni wimbo wake wa kwanza tangu alipotekwa na kuteswa kwa siku tatu.
Kupitia ‘Zimbabwe’ Roma amesimulia tukio la utekaji wake, watu anaoamini walimteka na sababu za kuamua kutoendelea kufuatilia jarada la upelelezi wa tukio hilo.
Mkali huyo pia amezungumzia kitendo cha baadhi ya wasanii wenzake kutomtembelea alipokuwa anauguza majeraha ya mijeredi ya watesi wake.
Pia, rapa huyo amezungumzia kauli ya Mbunge aliyedai bungeni kuwa amemtukana mkuu wa nchi.
- Video: Makonda kuwapa walemavu 200 miguu ya bandia bure
- Wagombea Sita Wa Urais TFF Uso Kwa Uso Kwenye Kipindi Maalum
Mkali huyo wa mashairi yenye mvuto wa maajabu (Rhymes of Magic Attraction) amekanusha tetesi kuwa watekaji wake walikuja na Noah huku akiwachana kuwa waachane na tabia za kutekana na kutumia silaha bali washindane kwa hoja.
‘Zimbabwe’ imerekodiwa ndani ya Tongwe Records chini ya upishi wa Bin Laden. Video inayoonesha muziki umehamishiwa maeneo ya malishoni imeongozwa na Nicklass.