Maamuzi ya chama cha soka nchini Ubelgiji ya kumtangaza aliyekua meneja wa klabu ya Everton Roberto Martinez kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo, yamepokelewa kwa hisia tofauti na mshambuliaji Romelo Lukaku.

Maamuzi ya kutangazwa kwa kocha huyo kutoka nchini Hispania, yalipitishwa na chama cha soka nchini Ubelgiji na kutangazwa katika vyombo vya habari usiku wa kuamkia hii leo, baada ya kamati ya utendaji kuafiki kwa pamoja juu ya suala hilo.

Akiwa katika benchi la kikosi cha Everton ambacho jana usiku kilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Man Utd, Lulaku alionekana kutokua mwenye furaha na alijaribu kuzungumza na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ubelgiji.

Kitendo cha mshambululiaji huyo mwenye umri wa miaka 23, kimejidhirisha katika moja ya clip za video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii ambazo zinaonesha Lukaku alipoteza furaha baada ya kusikia taarifa za Martinez kutangazwa kuwa kocha mkuu basdala ya Marc Wilmots.

Akiwa amekaa kwenye bechi la Everton, Lukaku alionekana kuweka mikono yake usoni. Alioneka kumgeukia Ross Barkley, na kumnong’oneza kitu, halafu Barkley akajibu ‘Hakuna jinsi’.

Vile vile Lukaku alionekana akimnong;oneza Mbelgiji mwenziwe Kevin Mirallas wakati wakitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Video: Steps Entertainment yapigwa faini mil. 7, Yapewa siku 7
Jeshi La Polisi Lamshikilia Rais Wa Klabu Ya Simba