Kundi la Rostam linaloundwa na Roma na Stamina, wanaotamba na wimbo unaoenda kwa jina la kijiwe nogwa wamefunguka kuwa Billnasi anapenda sana mapezi, kwenye video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikiwaonesha wakizungumzungumzia msanii huyo.

“Ni mdogo wangu ila ni ukweli kabisa, unajua hata sasa hivi waandaji wa show hawampigii simu Nenga ‘Billnass’ kumtaka kwenye show, huwa wanampigia Nandy na wanajua kabisa Billnass atamfuata nyuma kama sanamu” ameleeza Roma.

Billnass na Nandy wamekuwa wanatajwa sana siku za hivi karibuni kuwa wamerudiana japokuwa wenyewe wamekuwa wakikanusha kwenye baadhi ya mahojiano wanayofanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Aidha Roma na Stamina “Rostam” wameachia wimbo wao Audio na Video unaoitwa Kijewe Nongwa waliomshirikisha Nay Wa Mitego…, Bofya hapa kutazama

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=asDLszKL7-w]

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 23, 2019
MC Pilipili atangaza nia ya kuwania ubunge, ataja chama