Mkurugenzi Mtendaji na Mzalishaji wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amesema kuwa kitendo alichokifanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam juzi cha kuingia katika kituo cha hicho cha utangazaji, huku akiwa ameandamana na Askali Polisi ambao wa walikuwa na bunduki za kivita si kitendo cha kiungwana.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha 360, kinachorushwa na Clouds tv, amesema kuwa Makonda ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alipaswa kutoa taarifa hata kama kulikuwa na kipindi alichokuwa anataka kirushwe lakini si kwa kujichukulia maamuzi kama yale.

Ruge amesema kuwa Tasnia ya Habari inatakiwa kuheshimiwa na mtu yeyote na inafuata taratibu zote hivyo katika kitendo hicho si cha kiungwana.

“Makonda ni mtu wetu, ni rafiki yetu na tunafanya nae kazi kwa karibu sana, lakini katukosea sana inabidi atuombe msamaha, na tunalaani jambo hili,” amesema Ruge.

Aidha, amesema kuwa katika hatua ya maamuzi bado wanatafakari cha kufanya lakini hawataki kugombana na Serikali wala kiongozi yeyote, na ametoa wito kwa kiongozi yeyote mwenye ubunifu kwenda katika kituo hicho kupata nafasi ya kutangaza fursa zake.

Hata hivyo, Ruge amesema kuwa ni bora viongozi wakashirikiana vyema na vyombo vya habari ili kuweza kufikia maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Chelsea Yajizatiti Kwa Tiemoue Bakayoko
Tony Pulis: Wenger Atasaini Mkataba Mpya