Kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania Selemani Matola ameweka wazi mbinu waliyoitumia wakati Burundi wamesawazisha bao kwenye mchezo uliopigwa septemba nane mwaka huu ili kubadilisha matokeo na kuleta furaha kwa mashabiki na wadau wa soka nchini, ambapo mchezo huo ulikua wa kutafuta nafasi ya kushiriki kwenye kombe la Dunia litakalo fanyika nchini Qatar 2022.

Kwenye mchezo huo Taifa Stars ilifanikiwa kuifunga Burundi kwa mikwaju ya penati ambapo matokeo yalikua 3-0 na kufanikiwa kuingia hatua ya makundi katika kusaka nafasi ya kushiriki kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Baada ya kuifyeka Burundi, TFF yajipanga dhidi ya Sudan
Serikali kuwapeleka Israel wataalam 100 wa kilimo, mchakato wakamilika